Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiagana na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Bibi.Ritva Reinikka muda mfupi baada ya kufanya mazungumzo ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Kushoto ni Bwana James Adam Makamu Mstaafu wa Benki ya Dunia.Wakati wa Mkutano huo uliowashirikisha pia Wajumbe wengine kutoka serikalini na Benki hiyo viongozi hao walijadili kwa kina Mpango wa Kunusuru kaya Maskini kupitia mpango wa TASAF III.
Madhumuni
ya Mpango huu ni kuziwezesha kaya maskini kuongeza kipato,fursa na
kuimarisha lishe.Walengwa wa mpango huu ni kaya ambazo zinaishi katika
umaskini mkubwa katika mazingira hatarishi vijijini na katika shehia
upande wa Zanzibar.Mpango huu utatekelezwa katika kipindi cha miaka 10
chenye awamu mbili za miaka mitano kila moja.
Bajeti
ya utekelezaji wa mpango huu ni kiasi cha Dola za Marekani million
272.9.Mchango wa fedha hizo utatolewa na wadau mbalimbali ikiwemo
Serikali ya Tanzania amabyo itachangia kiasi cha Dola za Marekani
millioni 30, Benki ya Dunia Dola Za Marekani Millioni 220, DFID Dola za
Marekani 16,Serikali ya Hispania Dola za Marekani 6, na Shirika la
Misaada la Marekani(USAID) itachangia kiasi cha Dola za Marekani
900,000. Picha na Freddy Maro
No comments:
Post a Comment