Baadhi
ya wapishi katika hotel maarufu jijini Arusha wakiwa wanajadiliana
wakati Tamasha la watoto yatima na walemavu wa viungo likiwa linaendelea
ambapo siku hiyo ilikuwa imeandaliwa na chama cha wapishi duniani lengo
ni kuwaleta pamoja watoto.
Watoto waliofika katika tamasha hilo ambapo zaidi ya watoto 300 walishiriki kutoka sehemu mbalimbali jijini Arusha
Mtoto
Daudi Izrael Mshana mwenye ulemavu wa utindio wa ubongo(12)akiwa
amepakatwa na mama yake Belinda Izrael katika tamasha la watoto katika
hotel ya Mt.Meru jijini Arusha
Watoto wakiwa wanaimba nyimbo ya huzuni iliyokuwa imebeba ujumbe kuhusu watoto yatima
.Mustapha
na Ibraa Mhinda ni watoto waliokuja kujumuika pamoja na watoto yatima
ambapo kwa nyakati tofauti walitoa rai kwa jamii kuwathamini watoto
wanaoishi katika mazingira magumu ikiwa ni pamoja na kuwapa mapenzi
mema,malazi,mavazi,elimu na chakula bora
.Chef
Tom akiwa anaongelea juu ya tamasha hilo na vyombo vya habari ambapo
alisema kuwa jamii imesahau kwa kiasi kikubwa watoto wanaoishi katika
vituo vya kulelea watoto yatima pamoja na walemavu
Kushoto Mkurugenzi wa Bearfoot entainment Dorothy Mustapha akiwa anawakabidhi msaada wasimamizi wa vituo vya watoto yatima
Picha
ikimuonyesha msemaji wa World Chef day Chef Method Mrosso akiwa
anawakatia keki watoto wanaoishi katika mazingira magumu,mwishoni mwa
wiki jijini Arusha katika hotel ya Mt.Meru siku ambayo chama cha wapishi
duniani hujutolea kwa kuwapikia na kula pamoja
.Baadhi ya wapishi wakiwa katika picha ya pamoja .(Picha zote na Pamela Mollel wa jamiiblog.co.tz)
No comments:
Post a Comment