Friday, October 25, 2013

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA NCHINI JOHN CASMIR MINJA AFUNGA RASMI MKUTANO MKUU WA MAAFISA WAANDAMIZI WA MAGEREZA, MKOANI MOROGORO

  Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa hotuba ya ufungaji wa Mkutano Mkuu wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza uliomalizika leo Oktoba 25, katika Ukumbi wa Hoteli ya Edema, Mkoani Morogoro.
  Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(hayupo pichani) wakati akitoa hotuba ya ufungaji wa Mkutano Mkuu wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza uliomalizika leo katika Ukumbi wa Hoteli ya Edema, Mkoani Morogoro.
  Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(wa pili kulia) akitolea ufafanuzi baadhi ya hoja mbalimbali zilizojitokeza katika Mkutano Mkuu wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza kabla ya kufunga rasmi Mkutano huo leo Oktoba 25, 2013 katika Ukumbi wa Hoteli ya Edema, Mkoani Morogoro.
  Baadhi ya Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Morogoro wakiwakilisha Vyombo mbalimbali vya Habari hapa nchini wakifanya mahojiano mafupi na Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(kulia) mara baada ya kufunga rasmi Mkutano Mkuu wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza katika Ukumbi wa Hoteli ya Edema, Mkoani Morogoro.
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza waliosimama katika picha mara baada ya kufunga rasmi Mkutano Mkuu wa Maafisa Waandamizi wa Magereza Oktoba 25, 2013 katika Ukumbi wa Hoteli ya Edema, Mkoani Morogoro(wa pili kushoto) ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Haji Janabi(wa pili kulia) ni Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Alhaj Jumanne Mangara(wa tatu kulia) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa tatu kushoto) ni Kamishna wa Fedha na Utawala, Gaston Sanga. Wengine ni Mkuu wa Magereza Mkoani Morogoro, Naibu Kamishna wa Magereza, James Selestine na Mkuu wa Magereza Mkoani Tanga, Naibu Kamishna wa Magereza, Editha Mallya. Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza.

No comments:

Post a Comment