Mhe. Waziri wa habari, vijana utamaduni
na michezo Dkt Fenella Mukangara akisalimiana na Balozi wa Tanzania
nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini
Marekani.
Mhe. Waziri wa habari, vijana utamaduni
na michezo Dkt Fenella Mukangara akitia saini kitabu cha wageni kwenye
Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Balozi Watanzania nchini Marekani
Mhe. Mulamula na Afisa Habari wa Ubalozi, Mindi Kasiga wakiangalia.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani
Mhe. Liberata Mulamula akiwaongoza wageni wake Mhe. Waziri wa Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara na Katibu wa Wizara
hiyo kwenda kukutana na Maafisa wa Ubalozi kwenye ukumbi wa mikutano wa
kumbukumbu ya Mwl. Julius Nyerere.
Mhe. Liberata Mulamula, Balozi wa
Tanzania nchini Marekani na Mexico akimkaribisha rasmi Mhe. Waziri wa
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara kwenye
Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na kufanya Utamburisho kwa Maafisa
Ubalozi kujitamburisha kwa Mhe. Waziri kwa kutaja majina yao na nafasi
zao za kazi kwenye Ubalozi huo.
Maafisa Ubalozi wakimsikiliza Balozi wa
Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula wakati alipokua
akimtamburisha Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe.
Fenella Mukangara kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwl. Julius Nyerere
Mhe. Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akiongea na Maafisa wa
Ubalozi akiwapa salamu kutoka Tanzania na kuwaeleza mambo mbalimbali
yanayoikabili nchini yetu yakiwemo swala la wahamiaji haramu na jinsi
gani serikali inavyokabiliana nalo, swala lingine ni kuhusu ajira kwa
Vijana, juhudi anazofanya kuwaelimisha Vijana jinsi ya kujiajiri wenyewe
na pia alizungumuzia sekta binafsi kama zikifanya vizuri zitasaidia
sana maendeleo ya nchi yetu na kutilia msisitizo swala la michezo
mashuleni pia alielezea maswala ya vyombo vya habari na mchakato wa
rasimu ya katiba unavyoendelea hizi sasa Tanzania. Baada ya maelezo ya
Mhe. Waziri kulikuwa na kipindi cha maswali na majibu na kuchangia hoja
mbalimbali kuhusu maendeleo ya nchini yetu.
Kushoto ni Afisa Habari wa Ubalozi Mindi
Kasiga akifuatilia kwa karibu anachozungumuza Mhe. Waziri wa Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara, kulia ni Mhe.
Liberata Mulamula nae akifuatilia maelezo ya Mhe. Waziri kwa makini.
Mhe. Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo Dkt. Fenella Mukangara pamoja na Balozi wa Tanzania nchini
Marekani Mhe. Liberata Mulamula wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa
Ubalozi huo, kutoka kushoto ni Mwambata wa Jeshi Colonel Adolph Mutta,
Afisa Paul Mwafongo, Afisa Switebert Mkama, Afisa Agnes Lusinde, Afisa
Mindi Kasiga, Mhe. Waziri, Mhe. Balozi aliyesimama nyuma ya Balozi ni
Afisa Catherine Kijuu, Mkuu wa Utawala Mama Lily Munanka, Afisa Suleiman
Saleh, Afisa Emmanuel Swere Alfred na Afisa Abbas Missana.Picha Zote
Zimeletwa hapa naVijimambo Blog.
No comments:
Post a Comment