Ndege kubwa ya Fastjet ikiwa inaonekana angani wakati ikifanya survey juu ya uwanja wa kimataifa wa Songwe Mbeya.
Leo asubuhi majira ya saa Mbili na
nusu Ndege ya Fastjet kwa Mara ya kwanza kabisa ilishuhudiwa na watu
wachache katika Uwanja wa wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe ambapo ilikuwa
ikifanya Survey angani bila kutua.Ndege hiyo ambayo ilipita jirani kabisa na uwanja huo kwa Takribani ya zaidi ya mara tatu , ilifanya hivyo kwa sababu za kitaalam, hata hivyo hiyo ilikuwa ni amsha amsha huku siku chache zijazo ndege hiyo itatua kwa mara ya kwanza na Rasmi Jijini Mbeya katika uwanja wa Ndege wa Songwe.(P.T)
Kwa nyakati Tofauti Baadhi ya Abiria
waliokuwa wakijiandaa na kusafiri katika uwanja huo na Ndege zengine
walionekana kuwa na furaha na kuzungumza mambo tofauti ikiwa na pamoja
na kufurahishwa na hatua ya Ndege ya fastjet kuanza safari zake mkoani
Mbeya na kusisitiza kwamba itakuwa ni Mkombozi mkubwa kutokana na bei
zao kuwa chini na safari za uhakika.
Timu nzima ya Mbeya yetu Blog ilifika uwanjani mapema na kushuhudia kile kilicho onekana uwanjani hapo, na mpaka wanaondoka uwanjani hapo ndege hiyo ilikuwa tayari imesha anza safari za kurejea jijini Dar es salaam.

No comments:
Post a Comment