Mwenyekiti
wa taasisi ya sekta binafsi nchini Tanzania (TPSF) Dkt. Reginald Mengi
ambaye alikuwa ni mmoja wa watoa mada akizungumza na Sauti ya Amerika
kuhusu pendekezo lake la kusitishwa ugawaji wa vitalu amesema hilo
halikufanikiwa kwasababu kinachompa shida ni kwamba hakuna sera ya
kugawa au kutoa vitalu.
Aliongeza
kuwa wakati huo huo vitalu hivyo vinatolewa kwa wawekezaji wa kigeni,
alihoji katika mkutano huo kuwa inakuwaje wagawe rasilimali za taifa
bila sera maana ukifanya hivyo ni uporaji tu.
Alisisitiza
kwamba mtanzania hafaidiki na hajaona chochote cha kusema kwamba
mtanzania atawezeshwa kwasababu sheria ya mwaka 2004 inasema wazi wazi
kwamba watanzania watawezeshwa kumiliki uchumi wao.
Kuhusu
mazungumzo yake na katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini Bw.
Eliakimu Maswi amesema hakukuwa na makubaliano ya aina yeyote ni
mazungumzo tu , na tunapoendelea kuzungumza vitalu vinauzwa , kwahiyo
haoni kama kuna nia njema kushirikisha wazawa wa Tanzania katika sekta
ya gesi hasa katika ugawaji wa vitalu.
Kutokana
na kauli iliyotolewa na waziri wa nishati na madini Profesa Sospeter
Muhongo amemshauri arudi darasani akafundishe kwasababu anavyofikiria
watanzania siyo wanafunzi wake darasani akiongeza kuwa mawazo yake
hayana tija kwa wizara anayoongoza na wafanyabiashara wa Tanzania.
Kwa
mujibu wa Dkt.Mengi waziri huyo alikaririwa na vyombo vya habari nchini
humo akisema kuwa wafanyabiashara wa kitanzania wanajua biashara ya
kuuza juisi tu jambo ambalo alisema ni tusi.
Mkutano
huo ulifanyika kutokana na hatua ya hivi karibuni ya kugundulika kwa
mafuta na gesi nchini Tanzania. Waziri Muhongo akizungumza na waandishi
wa habari hivi karibuni alisema hakuna Mtanzania mmoja mmoja
atakayemiliki kitalu ila watanzania watawakilishwa na TPDC.Kusikiliza
mahojiano hayo ungana na idhaa ya kiswahili ya sauti ya Amerika. http://www.voaswahili.com/ content/article/1776533.html
No comments:
Post a Comment