Rais Jakaya Kikwete akipokea Mkuki wakati akisimikwa Uchifu
wa Kabila la Wabena na mmoja wa wawakilishi wa Wazee wa Kabila
hilo,kwenye wa Hafla ya Uzinduzi wa Mkoa wa Mpya wa Njombe.
Chifu Mpya wa Kabila la Wabena,Rais Jakaya Kikwete akiwahutubia wakazi wa Mkoa Mpya wa Njombe.
Chifu
Mpya wa Kabila la Wabena,Rais Jakaya Kikwete akiteremka Jukwaani baada
ya kusimikwa Uchifu wa Kabila hilo na kuwahutubia wananchi wa Mkoa wa
Njombe.
Rais
Jakaya Kikwete akipongezwa na Mkewe Mama Salma Kikwete baada ya
kusimikwa Uchifu wa Kabila la Wabena,wakati wa Hafla ya Uzinduzi wa Mkoa
wa Mpya wa Njombe.
Pongezi zikiendelea.
Machifu wa Kabila la Wabena wakiwa kwenye picha ya Pamoja.
Shangwe zilitawala wakati Rais Kikwete akibonyeza kitufe cha kuashiria Uzinduzi Rasmi wa Mkoa Mpya wa Njombe.
Rais Kikwete akizindua Vitabu.
Mamia ya Wakazi wa Mkoa wa Njombe wakiwaangalia vijana wa Halaiki wakati wakitoa Burudani uwanjani hapo.
Viongozi mbali mbali.
Rais
Jakaya Kikwete akisaini kitabu cha Wageni kwenye Banda la Sido wakati
apokuwa akitembelea mabanda mbali mbali kwenye Maonyesho ya Uzinduzi wa
Mkoa mpya wa Njombe.
Mmoja wa Watangazaji wa Redio akirusha Matangazo ya moja kwa moja kutokea Mkoani Njombe.
Rais Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakiangalia ngoma kutoka kwa vijana.
Rais Kikwete akisalimiana na Maafisa wa Sido
Rais Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Afisa wa TBS.
Rais Kikwete akitembelea Mabanda mbali mbali
Rais Kikwete azidua Kiwanda cha Chai Mkoani Njombe
Rais
Jakaya Kikwete akifunua kitambaa kwenye jiwe la msingi wakati akizindua
kiwanda kipya cha chai cha Ikanga, Njombe, ikiwa ni sehemu ya sherehe
za uzinduzi rasmi wa mkoa mpya wa Njombe Ijumaa Oktoba 18, 2013.
Rais
Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakisikiliza maelezo kabla ya
kuzindua kiwanda kipya cha chai cha Ikanga, Njombe, ikiwa ni sehemu ya
sherehe za uzinduzi rasmi wa mkoa mpya wa Njombe Ijumaa Oktoba 18, 2013.
Rais
Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakikagua chai ikichambuliwa
katika kiwanda cha chai cha Ikanga, Njombe, ikiwa ni sehemu ya sherehe
za uzinduzi rasmi wa mkoa mpya wa Njombe Ijumaa Oktoba 18, 2013.
Rais
Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakipata maelezo ya kiwanda kipya
cha chai cha Ikanga, Njombe, baada ya kukizindua ikiwa ni sehemu ya
sherehe za uzinduzi rasmi wa mkoa mpya wa Njombe Ijumaa Oktoba 18,
2013.PICHA NA IKULU
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
leo, Ijumaa, Oktoba 18, 2013, amezindua rasmi Kiwanda cha Kusindika Chai
cha Ikanga, Tarafa ya Lupembe, Wilaya ya Njombe katika Mkoa Mpya wa
Njombe.
Kiwanda
hicho kinachomilikiwa kwa asilimia 25 na wakulima wa chai wa Lupembe ni
ukombozi mkubwa wa wakulima wa Tarafa ya Lupembe ambao wamekuwa
wanakabiliwa na ukosefu wa sehemu ya kuuza chai yao.
Ufunguzi
wa kiwanda hicho cha Ikanga Tea Factory kinachomilikiwa na Kampuni ya
Ikanga Tea Factory Limited ni utekelezaji wa ahadi ya Mgombea Urais wa
Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati anafanya
kampeni ya Urais katika Tarafa ya Lupembe mwaka 2010. Ni kiwanda kipya
zaidi na bora zaidi cha kusindika chai katika Tanzania.
Ujenzi
wa kiwanda hicho ulianza mwishoni mwa mwaka 2010 baada ya Serikali ya
Rais Kikwete Mei mwaka huo huo kuiomba Kampuni ya Mufindi Tea and Coffee
Limited (MTC) kujenga kiwanda cha kusindika chai ya wakulima ambayo
sehemu yake kubwa ilikuwa inapotea na kuoza kwa sababu ya ukosefu wa
kiwanda.
Ili
kufanikisha ujenzi wa kiwanda hicho, MTC iliunda kampuni mpya ya Ikanga
Tea Company Limited Septemba 2010. Kampuni hiyo ni ubia kati ya MTC na
wakulima wa chai wa Lupembe ambao wanamiliki asilimia 25 za hisa za
kiwanda hicho kupitia umoja wao wa Lupembe Tea Farmers Trust.
Uzinduzi
wa leo ni awamu ya kwanza ya ujenzi wa kiwanda hicho. Chini ya awamu
hiyo ya kwanza yenye uwezo wa kusindika tani 1,800 za chai kwa mwaka kwa
kutumia njia moja ya uzalishaji iliyokamilika Juni mwaka jana kwa
gharama ya Sh. bilioni 3.75.
Awamu
ya pili ambayo inaendelea kujengwa, itagharimu Sh. bilioni 1.48 na
ikikamilika kiwanda kitakuwa na uwezo wa kusindika tani 3,500 na awamu
ya tatu na ya mwisho itagharimu Sh.bilioni 1.5 na kukamilika kwa awamu
hiyo kutakiwezesha kiwanda kusindika tani 5,000 za chai kwa mwaka.
Chini
ya uendeshaji wa Kiwanda hicho, chai yote ya wakulima inanunuliwa
kwenye vituo maalum na kusafirishwa kwenda kiwandani na magari ya
Kiwanda. Wakulima pia wanapewa mbolea kwa mkopo na wakulima wote wa chai
inayochukuliwa na kiwanda hulipwa kila mwezi kwa bei iliyopangwa na
Bodi ya Chai Tanzania.
Miongoni mwa mipango ya Kampuni ya Chai ya Ikanga ni kununua angalau hekta 600 za ardhi ili nayo ianze kulima chai ili kuongeza kiwango cha chai kinachozalishwa katika eneo la Lupembe na ukamilishaji wa shule kwa ajili ya watoto wa wakulima wa eneo la Lupembe.
Rais
Kikwete amezindua Kiwanda hicho ikiwa ni shughuli ya kwanza katika
shughuli nyingi ambazo atazifanya wakati wa ziara yake ya siku sita
katika Mkoa wa Njombe kuzindua na kukagua shughuli za maendeleo.
Miongoni mwa shughuli hizo itakuwa ni kuuzindua rasmi Mkoa wa Njombe.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
18 Oktoba, 2013
No comments:
Post a Comment