NILIPATA TUZO HII TOKA KATIKA MASHINDANO
YA KUMTAFUTA CHEF BORA WA MWAKA 2014 KWENYE NGAZI YA NUSU FAINALI KATIKA
MJI WA LINGKOPING NA FAINALI ITAFANYIKA MJINI STOCKHOLM TAREHE 7/2/2014
UKUMBI WA WATERFRONT.
TUZO HII NILIPATIWA NA ALIEKUA JAJI MKUU
WA MASHINDANO HAYO SIKU HIYO Chef Markus Aujalay PIA ALIFANIKIWA
KUWACHEF BORA WA SWEDEN MWAKA 2004 PIA NI CELEBRITY Chef ANAEMILIKI RESTAURANT NA AKIONGOZA KIPINDI MAARUFU CHA MAPISHI KATIKA TV SWEDEN MASTERCHEF.
Safari ilikua ni ya masaa 3 kutoka mji ninaoishi mpaka mji uliokua
mashindano yanafanyika namshukuru Allah nilikwenda na kurudi salama
amiin.
Katika picha hapo juu Chef Issa nikiendelea kutathmini Chefs wakiendelea kupambana
Huyu ndio alikua Jaji mkuu wa mashindano hayo ya nusu fainali siku hiyo anaitwa Chef Markus Aujalay Chef bora wa mwaka 2004 wa Sweden.
Ilitengwa sehemu maalumu ya sisi waalikwa kutathmini vyakula baada ya
kupangwa katika sahani na majaji kuonja na kutoa alam a ushindi.
Chef waalikwa wakiendelea kupata taswira za vyakula toka kwa chef washindani
Walijitaidi sana kwakweli kuonyesha ubora wao, safari bado ni ndefu na mashindano ni magumu sana
Taswira ya ukumbi toka kwa juu
Taswira ya meza kuu toka kwa juu
Taswira hii inakuhakikishia kua chef Issa alikua mweusi pekee katika
mashindano haya hivyo ilikua heshima kubwa sana kwangu na kwa taifa
langu kutambulika kwa uwezo wangu na mchango wangu na utaifa wangu mhhh
Viva Tanzania.
Utaratibu ulikua ukimaliza kuandaa chakula unaenda mbele ya kamera na
kuanza kujieleza kwa majaji na watazamaji waliokua wanaangalia live aina
ya chakula ulichotengeneza na mbinu ulizotumia
Upande wa pili ilikua ni maonyesho y vyakula ya chef waliopo huoni wenye
umri wa kuanzia miaka 13 mpaka 16. Pia makampuni maarufu y chakula na
yanayojihusisha na vyombo vya jikoni kama Electrolux, Santamaria, Arla
na mabingwa wa visu duniani Global pia walikuwepo kutangaza bidhaa zao.
No comments:
Post a Comment