Friday, October 25, 2013

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA NCHINI, JOHN CASMIR MINJA AFUNGA RASMI KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA IDARA YA MAGEREZA, MKOANI MOROGORO

  Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa hotuba ya Ufungaji wa Kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi katika Ukumbi wa Hoteli ya Edema, Mkoani Morogoro Oktoba 23, 2013.

  Baadhi ya Wajumbe Washiriki walioshiriki Kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Idara ya Magereza wakisikiliza hotuba ya Mwenyekiti wa Baraza Kuu Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(hayupo pichani) katika Ufungaji wa Kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi katika Ukumbi wa Edema, Mkoani Morogoro Oktoba 23, 2013.

  Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akimkabidhi Begi lenye makabrasha ya Kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Idara ya Magereza Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulwakil(kulia) mara baada ya kufungua rasmi Kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Idara ya Magereza katika Ukumbi wa Edema, Mkoani Morogoro.

Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wajumbe wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi raia wa Idara ya Jeshi la Magereza mara baada ya kufunga rasmi Kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Idara ya Magereza Oktoba 23, 2013 katika Ukumbi wa Edema, Mkoani Morogoro. Wa pili kulia ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa, wa kwanza kulia ni Kamishna wa Fedha na Utawala, Gaston Sanga(wa kwanza kushoto) ni Mwenyekiti wa Tawi la TUGHE-Idara ya Magereza, Bw. Sedumba Katemba na wa pili kushoto ni  Katibu wa Baraza la Wafanyakazi - Idara ya Magereza, Bi. Radegunda Mchau. Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza.

No comments:

Post a Comment